Ubunifu Kazini

Ubunifu Kazini
January 14, 2018 Mark Tedford

Kuwapa wafanyakazi wako kuwa na uhuru wa kuunda hisia chanya sehemu ya kazi kunaweza kuboresha maadili na ukaaji wa muda mrefu kwa wafanyakazi.

Leo ningependa kuzungumza na wafanyabiashara na mameneja kwa kuuangalia mwili wa binadamu ulivyoumbwa ili kutupatia uelewa wa wafanyakazi wanavyoweza kufanya kazi. Naamini kwamba mwili wa binadamu umeumbwa kufanya kazi na mwanadamu ameumbwa na hisia za kufanya kazi. Aristotle aliamini kwamba kazi ilikuwa ni adhabu kutoka kwa miungu. Katika jamii ya Kigiriki anasa ilisifiwa na kazi ilionekana kama kitu ambacho kisichokuwa na utu.

Naamini kwamba mtu aliumbwa kufanya kazi ili kazi iwe afya kwetu. Katika mwaka 2006, Idara ya kazi na mafao ilionyesha, kwamba, kulikuwa na uhusiano kati ya afya njema na kufanya kazi. Pia kura za maoni ya Gallup zinaonyesha uhusiano kati ya msongo wa mawazo na ukosefu wa kazi. Wafanyakazi ambao walikuwa hawana ajira kwa zaidi ya wiki 27 walionekana mara tatu zaidi kupata ugonjwa wa msongo wa mawazo. Zaidi kuliko wale waliokuwa wakifanya kazi kimwili tu. Watu wanahisia za kujisikia kwamba wanachokifanya kina ubunifu na kina maana. Maslow alisema hitaji kuu la mwanadamu ni hitaji la kujitambua.

Watu wengi wanatambua kuridhika kunaletwa na mtu kuwa ubunifu. Kwa bahati mbaya watu wengi ni wabunifu katika mambo wanayoyapenda kuliko katika  kazi. Nafikiri kila mmoja anapaswa kujiona yeye ni mbunifu akiwa kazini na siyo tu kama mfanyakazi.
Dorothy Sayers alinukuliwa akisema kwamba mtu mbunifu huishi akifanya kazi anayoipenda, kwa upande mwingine mfanyakazi anaishi kwa kufanya kazi anayoidharau. Ukosefu wa ubunifu katika kazi unatunyima kuwa na hali ya heshima. Na, nafikiri wafanyabiashara na mameneja wanapaswa kujitahidi kuunda kazi ambazo zitaruhusu wafanyakazi kujitegemea na kufanya kazi kwa ubunifu. Ubunifu na kujitambua kazini kunaruhusu ushiriki zaidi. Na hilo ni jambo ambalo mfanyakazi wa Kimarekani hajafanya kazi nzuri bado. Maoni ya hivi karibu wa Gallup yanaonyesha kwamba 33% tu ya wafanyakazi wanashiriki katika kazi zao.

Baadhi ya kazi ni rahisi kuona jinsi ambavyo mfanyakazi anaweza kuwa mbunifu au kufanya kazi iwe na maana. Msanii kwa mfano ni mbunifu muda wote katika kazi zao.
Na daktari anaonekana kitamaduni kama mtu muhimu sana. Kwa hiyo, kwa asili wanahisi kwamba kazi zao zina maana. Lakini siyo kila kazi ipo hivi. Baadhi ya kazi zinaonekana kama siyo muhimu katika utamaduni wetu, na baadhi ya kazi ni vigumu kuona jinsi gani unaweza kuwa mbunifu. Kwa mfano mtu anayefanya kazi ya kupokea simu kwenye biashara yako kama mhuduni. Ni vigumu kuona jinsi wanavyoweza kuwa wabunifu katika kazi zao.

Nafikiri kwamba kila kazi inaweza kufanywa katika njia ambayo inagusa ubunifu wa mfanyakazi. Mfano mzuri ni mhuduni wa hotelini. Hii huonekana kama kazi isiyo na umuhimu na ambayo haimfanyi mtu kuwa mbunifu. Lakini wengi wenu mumewahi kwenda kwenye hoteli nzuri ambapo unapoingia chumbani, unakuta mhuduni amekunja taulo katika umbo la ndege. Wanajali kazi zao, na wanataka ujue kwamba wanajali kazi wanayoifanya. Kama wameweza kutoa huduma ya kukunja taulo kwenye umbo la ndege, hivyo inaonyesha wameweza pia kusafisha sehemu zingine za chumba.

Mfano mwingine wa hili ni mtu anayezungusha matangazo. Wengi wenu mmeshaona sehemu mbali mbali za kona za mitaa, wafanyakazi wakibeba matangazo kwa ajili ya biashara za rejareja. Siwezi kufikiria kazi mbaya au kazi yenye kuchosha kama kusimama nje kwenye jua kali ukibeba tangazo. Hivi karibuni nilikwenda Vegas na walikuwa na “mashindano ya wabeba matangazo”, ambapo walishindana kuona mtu ambaye ni bora na mbunifu zaidi katika kuzungusha matangazo yao.

Nafikiri ambapo wafanyakazi wanapokuwa wabunifu kila mmoja anakuwa mshindi. Wafanyakazi wanakuwa washindi kwa sababu wanafurahia kazi zao, na wanaonyesha ujuzi wao kupitia kazi zao. Mwajiri anashinda kwa sababu anaye mfanyakazi ambaye anajishirikisha, na wateja wanashinda kwa sababu wanapata burudani na kutosheka kwa kazi ambazo wafanyakazi wanazifanya. Mwajiri anapaswa kutoa ruhusa kwa mfanyakazi kuonyesha ujuzi wake katika kazi na kuwa wabunifu. Na hata tafuta njia ambazo zinatoa zawadi kwa tabia za ubunifu. Waulize kitu gani cha ziada ambacho kinatenganisha kazi ya utaalamu na isiyo na utaalamu. Na hicho ndicho kinatenganisha kati ya wasanii na mtu wa kawaida. Sasa ukijua hilo litakupelekea kupata njia ya kuweza kuwa mbunifu katika kazi yako.

Mark Tedford

0 Comments

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

Share This

Share This

Share this post with your friends!