What Is IBB Talks?

IBB Talks ni kitu gani?

IBB Talks ni taasisi inayojihusisha na  kuhamasisha uanzishwaji, ukuaji na uendelezwaji wa biashara ndogo ndogo

Lengo letu kubwa ni kueneza ukweli usiopitwa na wakati ulimwenguni kote na usiokuwa na mipaka ya kitamaduni ama hali Fulani ya uchumi.

Habari. Naitwa Gary Shotton. Napenda kukueleza kuusu dhana ya kuanzishwa kwa tovuti hii- na natumaini mtazamo mpya- uitwao  IBBTalks.com.

Inatumia mtindo unaofanana na wa tovuti nyingine iitwayo Ted Talks inayopatakina kutoka TED.com. Ni tovuti maarufu sana. Wana mazungumzo yasiyozidi dakika ishirini kuhusu karibu kila mada muhimu. Maelfu ya watu wanafungua na kutazama  tovuti ya TED Talks. Maelfu ya watu huhudhuria mikutano ya TED Talks. Mada zao nyingi zinahusu kuokoa nyangumi na taaluma; elimu ya ubongo na kuruka kwa ndege. Mada yeyote unayofikiria inapatikana TED Talk na unaweza kumskia mtaalamu wa kitengo hicho akiiongelea.

Jamii zetu ni kama vile zinaelekea upande huo. Hatuvutiwi sana na barua pepe ama ujumbe mfupi wa mtandao wa kijamii wa twita. Tunahitaji mawazo ya msingi ambayo tunaweza tukatumia. Natumaini kufanya haya kupitia IBBTalks.com.

Yazingatie haya na uyatumie kwa kile niitacho kichwa cha habari “mafunzo ya kujenga biashara yenye maadili na faida” Kuna njia za kutengeneza faida bila kuzingatia maadili. Hivyo sio vyema. Ukweli utajulikana mwishoni. Kama hukuzingatia maadili kuna mtu atagundua. Anaweza kutoka katika familia yako ama mfanyakazi mwenzako wa karibu. Hivyo nataka kuwasisitiza  juu ya kuzingatia maadili na kanuni za kibiashara.

Lakini kwanini tusiwepo katika biashara isiyo na mvuto na kuleta faida. Kipimo cha utendaji katika biashara ni faida. Faida huonyesha kama umeshinda au haupo katika ulimwengu wa kiuchumi. Ndiyo, sasa upo katika harakati za kusaidia watu. katika harakati za kujenga maisha na kuelimisha uongozi.Lakini ukiwa kwenye biashara unatakiwa kuchunguza faida yako. Hayo mambo mengine yote hayana faida kwenye kujenga biashara.

Hivyo, natumaini kuwa na mafundisho ya kujenga biashara yenye maadili na faida. Kwa sasa, hainitegemei mimi bali nazindua. Yamkini nakwenda kuwapatia video hamsini mtakakazojifunzia kwa kutazama na kusikiliza. Tunakwenda kuzigawanyisha hizo video katika makundi na mada mbali mbali. Baadhi zitakuwa kama ni mafundisho ya kiroho lakini mafundisho mengi hayatakuwa mahubiri ya Biblia. Shauku yangu ni kuwa haya mafundisho yawe na msingi wa kibiblia kwa sababu maadili msingi wake ni Biblia.

Nakuomba uwe msemaji kama una ujuzi katika hili na mimi nitalifanyia kazi. Na hasa kama  unamiliki biashara na una uzoefu wa miaka mingi katika biashara. Hatuhitaji nadharia wala usirejee katika kitabu cha mtu mwingine bali tunahitaji wewe ujizungumzie mwenyewe.

Katika video nyingne utanisikia mimi lakini kwa kifupi, nikiwa nmekaa katika karakana yangu. utamuona mfanyakazi nyuma yangu. kila mwezi nalipa wafanyakazi wangu mishahara kiasi cha dola 50,000. Kila wiki nanunua vifaa vipya vyenye thamani ya dola 700,000 kwa kila mwaka. Nina wafanyakazi sitini na tano na siyo kwamba najisifia. Kuna watu wenye uwezo hata zaidi ya mara kumi ya vitu nilivyonavyo. Sipo katika mashindano ya kupata zaidi bali nawajali tu wateja wangu. Ni kwamba tunatimiza dhamira tuliyojiwekea ya kujali wateja wetu.

Tunatafuta watu wenye maono kama yetu na wenye uwezo wa kuzungumza na sisi. Tunatarajia kupata ladha za kimataifa. Kwa hivyo tunapoongelea mfunzo ya kujenga biashara yenye maadili na faida, siyo Marekani pekee. Ni pamoja na Mexico, China Mongolia, Ujerumani, na Austria. Maono yetu ni kutafsiri mazungumzo haya katika lugha mbali mbali.

Huwa nasafiri mara nne au tano kwenda nchi mbalimbali. Naenda Mexico na China kila mwaka na kuwaalika watu wenye misingi ya kibiashara, kidini na Kimaadili kwa ajli ya kutoa mafunzo.  Kwa hivyo video zangu binafsi zitatumiwa na wengi na huu ndo mpango wangu na moyo nilionao.

Ni shauku yangu kuwa tutaweza kusaidiana na pia kuona ni jinsi gani dunia ilivyo ndogo. Kanuni zile zile zitakazotumika kujenga biashara yenye maadili na faida leo katika nchi za Marekani zaweza kutumika hata miaka kumi ijayo katika nchi yeyote duniani. Pia zilitumika miaka ishirini iliyopita katika nchi yeyote duiani. Na hizi ndio kanuni za msingi tunazotarajia

Natumai umepata uelewa kuusu nini tunaongelea katika IBB Talks na kwamba utavutiwa kutusikiliza. Pia utajisajili ili uweze kupata mafunzo haya kila mara. Natumaini baadhi yenu wenye uzoefu mtaguswa kututumia video zenu. Ndio kwanza tunaanza na ni kazi ya muendelezo. Hivyo, ni matumaini yetu kuwa mtajumuika nasi.

 

 

Share This

Share This

Share this post with your friends!