IBB Talks Speakers

Wafikiriaji. Watendaji. Mawakala wa Mabadiliko

Kama ni mtu wa majira, ni mfanyabiashara mwenye uzoefu na ungependa kushirikisha wengine maarifa yako, unaweza kutuma video yako kwa mazungumzo ya IBB Talks.

Angalia video ifuatayo ili upate maelezo ya jinsi ya kutuma video kwa ajili ya kuzingatiwa kwenye mazungumzo ya IBB Talks.

[vimeo 166751483 w=100 h=563]

Maswali anayouliza mzungumzaji

1.  Je mazungumzo yanapaswa kuwa ya muda gani?

Mazungumzo mazuri yanawakilisha wazo kuu kati ya dakika 7 hadi 9.

2. Je kuna somo maalumu?

Tunatafuta mazungumzo ya biashara ambayo yana msingi wa   Kibiblia kwa ujumla

3. Je, naweza kutumia mifano maalumu ya biashara?

 Wazungumzaji wanatarajiwa kuhusisha mifano binafsi ili kuonyesha uzoefu wao unaohusiana na somo wanalolizungumzia. Hakikisha mifano isipungue 30%  ya mazungumzo.

4.  Je kuna mfumo katika maudhui?

 Tumegundua kwamba dhana 1. Waambie wasikilizaji kile ambacho unataka kuwaambia katika sekunde 15-20 za kwanza. 2. Waambie mada kuu ya mazungumzo yako kwa dakika 6-7 na mwisho 3. Waambie kile ambacho ulichosema kwa kufunga sekunde 15 hadi 20 kwa kifupi.

5.  Je  napaswa kuongelea uzoefu wangu au wa watu wengine?

Epuka kufundisha mafundisho ya watu wengine, kutumia mwongozo au kitabu kilichoandaliwa na mtu mwingine

6. Je ujuzi wa kutia moyo unahitajika?

Katika uzoefu wetu, elimu ya kutia moyo inatokana na kujifunza jinsi wengine walivyoweza kupata mafanikio katika ulimwengu wa biashara, na siyo kwa sababu mzungumzaji anao ujuzi katika kutia hamasa.

7. Je kuna kikomo cha umri?

Hakuna kikomo cha umri, lakini wazungumzaji vijana haswa wanapaswa kujiandaa kueleza historia ya biashara na kiwango cha uzoefu.

8. Je kuna kitu kisichokubalika?

 Hili si jukwaa la kuajiri wengine kwa ajili ya mpango wako wa biashara au mfumo wa piramidi

9. Any Technical Guidelines for Video and Sound quality?

Video lazima iwe na ubora wa HD720 au juu zaidi

Video ya picha ya mzungumzaji lazima ipigwe karibu ili kuonyesha uso.

Sauti inapaswa kuwa safi na ubora wa LAV.

Kipaza sauti kinaruhusiwa kama kitakuwa karibu kabisa na mzungumzaji

Viwango vya sauti havipaswi kuwa vipande. Fanya viwe katika -6db au chini.

Video ya mwisho inahitajika kutumwa katika mfumo wa  mp4 au mov

10. Je kuna ushauri wa jinsi ya kurekodi video?

Jiandae! Tunaweza kupiga picha za video nyingi kadri iwezekananyo katika wakati wetu.

Unapokuwa umejiandaa vizuri katika mazungumzo yako, na sehemu ulipo, itaharakisha upigaji wa picha za video.

Andaa mafundisho yako kabla,  itakusaidia katika mtitiliko wa uzungumzaji, itakuwa rahisi na haraka kuhariri.

Piga picha ya video sehemu ambayo inaonyesha biashara yako

Kwa mfano kama una biashara ya mgahawa, jaribu kupiga picha ya video jikoni au jiko likiwa nyuma yako

  Watu wanapoonekana wakifanya kazi kwa nyuma inaleta hamasa kwenye picha ya mazungumzo yako, hii inafanya biashara yako kuwa na msisimko zaidi.


Kama ungependa kushiriki kwa kutuma video ya mazungumzo yako, tafadhari wakilisha kupitia kwa kujaza fomu. Kama utapata ugumu wowote katika kututumia video yako, maswali yeyote, au maoni tafadhari yatume kwa kupitia barua pepe: info@IBBTalks.com

Asante!

Ukitaka kuangalia video fupi ya maelezo ikielezea jinsi ya kutuma mafundisho ya video kwa ajili ya kuzingatiwa.

 

Share This

Share This

Share this post with your friends!